Marekani imesema kuwa imetamaushwa
na hatua ya viongozi wa Palestina ya kutaka kujiunga na mahakama ya
kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC.
Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani inasema kuwa hatua hiyo itachochea uhasama na kwamba haitaafikia malengo yake yoyote.Israel tayari imeonya kuchukua hatua za kujibu mpango huo.
Ramani ya eneo la Gaza linalozozaniwa kati ya palestina na Israel
Hatua hiyo ya Palestina ya kutaka kuwa mwanachama wa ICC huenda ikatoa fursa ya uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu wa kivita dhidi ya Israel katika eneo la Gaza na West Bank.
Waandishi wanasema kuwa hatua hiyo pia huenda ikasababisha makundi ya wapiganaji kama vile Hamas kushtakiwa.