Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar
Kheri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tagi mpya ya Shirika la
Bandari Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza miaka
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar
Kheri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tagi mpya ya Shirika la
Bandari Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza miaka
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Tagi
iliyozinduliwa ikirusha maji ikiwa ni majaribio ya kuzima moto iwapo
tatizo hilo litajitokeza. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………
Na Miza Kona Na Abdalla Ali – Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri amewataka
wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar kufanya kazi kwa juhudi na
ufanisi kwa lengo la kuleta maendeleo na mabadiliko nchini. Hayo ameyaeleza huko katika
Shirika la Bandari Zanzibar wakati akizindua Tagi mpya ya Shirika hilo
MV Shuwari ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kusherehekea miaka 51
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema bandari ni chachu ya
maendeleo katika nchi yoyote Duniani na muhimili mkuu wa kuleta
maendeleo na mabadiliko yatakayofanywa kwa ufanisi na juhudi kubwa
zitakazoweza kuinua uchumi wa nchi. Amefahamisha kuwa utendaji wa kazi
unategemea rasilimali watu na vifaa vya kisasa vinavyo kwenda sambamba
na mazingira ya kazi yatakayoleta maendeleo na mabadiliko ya haraka
katika kutoa huduma za utendaji.
“Utendaji wa kazi unategemea
rasilimali watu na vifaa vya kutosha na vya kisasa ambavyo vinakwenda
sambamba na mazingira ya kazi ambavyo vitaleta maendeleo na mabadiliko
ya haraka katika kutoa huduma za utendaji”, Alieleza Waziri Omar.
Aidha Waziri Omar ameeleza kuwa
ufinyu wa nafasi ya kuhifadhia mizigo bandarini hapo, pamoja na
Wafanyabiashara kutoondosha Makontena yao kwa wakati ndio changamoto
kubwa zinazoikabili bandari hiyo.
Waziri Omar pia amewataka
wafanyabiashara kuchukua juhudi za kutoa mizigo yao bandarini kwa wakati
ili kuondosha msongamano uliopo na kulipa ushuru wa mizigo hiyo ili
kuliongezea pato la Taifa. Amesema madhumuni ya Tag hiyo ni
kuimarisha ufungaji na ufunguaji wa meli bandarini hapo hivyo mategemeo
makubwa ni kuona kuwa inatumika ipasavyo kwa kufuata ushauri na
maelekezo ya wataalamu kwa lengo la kuleta maendeleo ya bandari na taifa
kwa ujumla.
Nae Mkurugenzi mkuu wa Shirika la
Bandari Zanzibar Cpt. Abdalla Juma Abdalla amesema Tagi Mv Shuwari
tayari imeshaanza kazi ya kusaidia kufunga na kufungua meli gatini
ambayo inauwezo wa kukabiliana na majanga ya moto pamoja kusaidia
kuokoa maisha ya watu inapotokea ajali ya meli au boti baharini.
Amesema Tagi hiyo imejengwa kwa
udhamini wa kampuni ya Damen Shipyards ya Uholanzi kwa kushirikiana na
Shirika la Bandari la Zanzibar na imegharimu Tsh.zaidi Bilioni 10 ambapo
Bilioni 6.9 ni mkopo kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na ghrama
zilizobaki zimelipwa na Shirika la Bandari.
Tag hiyo ina urefu wa mita 22.64,
upana mita 7.84, kina cha kueleya mita 3.50, nguvu zake 2720 HP, mwendo
11.70 knots, nguvu za kuvuta tani 38, na uzito wa tani 140 inatarajia
kuleta maendeleo makubwa bandarini hapo.
na JIACHIE BLOG