Jan 8, 2015
Simulizi ya Kweli: Miguu Yangu Iliungua na Moto-Esha Buheti
Ukimuona mtu mzima ujue kapitia mengi kisome hapa kisa cha mrembo na mwigizaji wa filamu hapa Bongo, Esha Buheti kuungua na moto miguuni. Esha anaeleza..
Tarehe kama ye leo (jana) nikiwa nipo darasa la nne nakumbuka nimetoka shule nikawa naenda mtoni kuchota maji , wakati naelekea mtoni njiani nikaona sehemu imetulia kuna kama mchanga mweupeee kwakua nilikua sijui akili ikaniambia ule ni mchanga wa beach.
Nikaacha kufata maji nikaenda mpaka pale kwenye ile sehemu nikawa najiuliza hiki nini wakati natafakari, nikajikuta naanza kutembea kuelekea kwenye ule mchanga kumbe haikua mchanga ilikua jivu la moto lililotakana na mapumba ya mpunga yaliochomwa bila kujua nkawa naendelea kumbe mbele kuna shimo lenye mapumba yenye moto nikadumbukia nikaanza kuskia maumivu ya moto nikaungua sana miguu yangu......
Niliungua vibaya sana niliuguzwa vidonda vikapona baada ya mwezi mzima..... Ila makovu yalibakia miguuni mwangu kuna siku nipo mitaa ya Mwenge(Dar) natengeneza kucha akapita Mmasai akaniona akanambia ana dawa yakutoa makovu ya moto sikumuamini, ila akaniambia itakuponya basi nikanunua nikaanza kutumia .
Leo hii naitazama miguu tangu hata siamini.......(Kama inavyoonejkana kwenye picha hapo juu) Ila kuna kovu bishiii ilooo limegoma kutoka but naridhika na hali yangu niliokua nayo.....
Esha alimalizia na msemo huu.
“Ridhika na ulichojaaliwa nacho Mungu ila jifunze kua kama upo hai jua kabisa bado unaendelea kuumbwaa”.
Pole sana, Ujumbe umefika.