Mwigizaji wa filamu za Kibongo Jennifer Kyaka ‘Odama’, amedai kuwa
mwanaume ambaye anaweza kumuoa jambo la kwanza lazima atambue kuwa yeye
anafanya filamu kwa muda mrefu hivyo hawezi kuacha kazi yake kwa sababu
ya kuingia kwenye ndoa.
Odama alifungua kinywa chake baada ya kuzungumza na paparazzi wa GPL,
ambapo alidai kuwa haiwezi kutokea kuacha kufanya filamu ili amridhishe
mwanaume kwani maisha yake yamekuwa yakiendeshwa na kazi hiyo kwa muda
mrefu.
“Naamini kuwa yule ambaye atakuja kwa nia ya kunioa kwanza lazima
atambue kuwa nafanya filamu, sitahitaji anieleze jambo la kuacha kazi
yangu, mimi ni mwanamke ambaye nahitaji kupata maendeleo kupitia kazi
zangu,” alisema.
Picha:Odama akiwa na mtoto wake.
BONGO MOVIES.COM