Chama cha gofu nchini Tanzania (TGU)
kimesema kuwa kitashiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika huko Rio
de Janeiro, Brazil mwakani.Gofu itashiriki kwa mara ya kwanza katika
michuano ya Olimpiki tangu michuano ya mwaka 1904 ilipofanyika.
Ushiriki
wa mchezo huo, ambao utajumuisha wachezaji wanawake na wanaume katika
michezo ya mmoja mmoja (individual team) kutoka katika nchi
zitakazofuzu, ulipokelewa kwa shangwe na wadau wa mchezo huo kutoka nchi
mbalimbali duniani, ikiwemo Tanzania.‘Tumejiandaa kwa muda mrefu na zaidi ya vijana 60 kutoka vilabu mbalimbali nchini wanaandaliwa ili kupata timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya kufuzu”, alisema makamu wa raisi wa TGU, Joseph Tango
Rwanda itakuwa mwenyeki wa michuano ya Afrika ya Mashariki (kanda ya 5) itakayokuwa ni sehemu ya kufuzu na raisi huiyo wa TGU, Tango amesema Tanzania inategemewa kusafiri kwenda Kigali kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika tarehe 27-30 mwezi wa kumi.