Kikosi kizima cha timu ya Yanga
Yanga imeng'oka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa bao 1-0 na JKU.
JKU
inayomilikiwa na Jeshi la Zanzibar imefanikiwa kuing'oa Yanga katika
mechi kali na ya kuvutia kwenye Uwanja wa Amaan, huko Zanzibar.Muuaji wa Yanga alikuwa Amour Mohammed ambaye alifunga bao hilo adhimu kabisa katika dakika ya 72 na kupeleka simanzi Jangwani,kitendo kilichoivuruga Yanga wasionane na kushindwa kusawazisha ,ingawa watoto hao wa Jangwani watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi kadhaa za kufumania nyavu bila mafanikio katika kipindi cha kwanza.
Kutokana na ushindi huo, sasa JKU itacheza nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo iliing'oa Azam FC .