Bosi wa timu ya Chelsea Jose
Mourinho ameshtakiwa na shirikisho la kimataifa la soka FA kwa madai
yake kwamba kuna kampeni ya chinichini inayofanywa na marefa dhidi ya
timu yake
Kauli hiyo ya Mourinho aliitoa baada ya kutoridhishwa na
penati ilisababisha timu yake itoke sare ya moja moja na Southampton
,mwezi uliopita mnamo tarehe 28.Mourinho ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu na amepewa muda mpaka tarehe 13 ya mwezi huu kujibu tuhuma zinazomkabili.