kiungo wa timu ya Manchester City
Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kutajwa na shirikisho la soka
barani Afrika kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa mwaka wanne mfululizo.
Toure
ana umri wa miaka 31,aliteuliwa baada ya kucheza kwa kujitoa na kuleta
ushindi katika Premier League na League Cup, na pia alijitoa kuisaidia
Ivory Coast kuingia katika kombe la mataifa ya Africa yatakayo fanyika
baadaye mwaka huu.Toure amewapiku mshambuliaji kutoka Gabon, Pierre Emerick Aubameyang na golikipa mnigeria Vicent Enyeama.Toure pia alikwaa tuzo ya FIfa ya Ballon D'Or mwezi wa kumi mwaka wa jana..