Taarifa iliyoifikia
Malunde1 blog hivi punde,inaenleza kuwa Bondia maarufu hapa
nchini,Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha Miaka mitatu (3) jela kwa
kukutwa na hatia ya kumpiga na kumjeruhi Meneja wa Bar yake iliyopo
mjini Morogoro.
Cheka alifikishwa
kizimbani leo na kusomewa mashtaka ya kushambulia na kuzuru
mwili,akidaiwa mnamo julai 02 mwaka 2014, bila uhalali na akijua kufanya
hivyo ni kosa kisheria, alimpiga kwa ngumi maeneo ya kichwani na
tumboni, Bahati Kabanda maarufu kama Masika, na kumsababishia maumivu
makali.
Hukumu hiyo imetolewa leo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi,Mkoani Morogoro.