Elizabeth Michael, ‘Lulu’
Mrembo na muigizaji wa filamu za kibongo, Elizabeth Michael, ‘Lulu’
amesema wasanii wengi wa filamu hawana mawazo ya maana na
hawafikiriimambo makubwa kuhusu wanachokifanya. Bali hufanya tu kwa
sababu wapo katika jamii na ahahisi wale wa bongo fleva wanafikiri
zaidi yao“ Unawaza kwanza kIsha unatenda, wasanii wa filamu hatuna mawazo mazuri zaidi ya ubishoo tu, hatuoni mbali hatuna wivu wa kimaendeleo leo unakuta msanii wa Bongo Fleva wanatoka nnje na wanarudi na tuzo lakini sisi tumekaa tu".alisema Lulu.
Lulu amesema mwaka huu atapigana na kuhakikisha anatoka kimataifa na kufanya kazi kubwa na kufungua njia kwa wasanii wa filamu walio bweteka na kuridhika na soko la ndani ambalo halieleweki