Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC, Dr. James Mataragio akiongea katika mkutano wa mwaka
wa GE Oil & Gas uliofanyika Florence, Italy
Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (aliesimama katikati)
akibadilishana mawazo na CEO wa Exxonmobil (Moja ya Kampuni kubwa ya
Mafuta na Gesi duniani). Aliesimama sambamba na Waziri ni Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC, Dr. James Mataragio na aliekaa ni Rais na CEO wa GE
Oil & Gas, Lorenzo Simonelli.
Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (MB) akisikiliza kwa
makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. Mataragio (Hayupo
pichani) akiongea kuitangaza Tanzania kwa wadau na wawekezaji wakubwa wa
Mafuta na Gesi duniani, aliekaa kushoto kwa Waziri ni Rais na CEO wa GE
Oil & Gas, Lorenzo Simonelli.
Waziri
wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (MB) akihutubia wadau
mbalimbali wa mafuta na gesi duniana katika mkutano wa mwaka
ulioandaliwa na GE Oil & Gas uliofanyika Florence, Italy.
…………………………………………………………………………………………
Pamoja
na kuwepo kwa changamoto za kushuka kwa bei ya mafuta duniani, Tanzania
bado imeendelea kuvutia wawekezaji kutoka pande zote za Dunia kuja
kuwekeza katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini. Akiongea
katika mkutano wa mwaka wa GE Oil & Gas, Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. George Simbachawene (MB) aliwaalika wawekezaji wakubwa
kutoka pande zote za dunia kutembelea Tanzania na kuona nafasi za
uwekezaji zilizopo.
Mkutano
huo uliofanyika Florence, Italy uliwakutanisha wadau wakubwa wa Mafuta
na Gesi duniani kujadili changamoto katika sekta hiyo na namna ya
kuzikabili. Kauli mbiu ya mwaka huu ililienga zaidi kuangalia namna
ambavyo sekta hii itachochea maendeleo ya dunia nzima kwa kuhakikisha
kuwapo kwa nishati endelevu na yenye kujali mazingira.
Tanzania
iliwakilishwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. James Matargio
ambaye alipata fursa ya kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha fursa zilizopo
katika sekta ya Mafuta na Gesi nchini. Dr. Mataragio alisema “ pamoja
na kuwa bei za mafuta zinaendelea kushuka, bado kuna fursa ya kutumia
gesi kusaidia upatikanaji wa nishati endelevu na yenye kulinda mazingira
kwa vizazi vya sasa na baadae”
na JIACHIE BLOG