Mkuu
wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akisalimiana na Muwakilishi wa
kampuni ya Airtel mkoa wa Shinyanga,Ezekiel Nungwi wakati Kampuni hiyo
ilipofika kuwaona wahanga wa mafuriko na kuwapelekea Baadhi ya Vitu
mbali mbali.kampuni hiyo ya Airtel imetoa,sabuni ,mabati ,maharange
,mchele ,mafuta kwa Wahanga hao.
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akiwapongeza wafanyakazi wa
Kampuni ya Simu ya Aitel kwa moyo wao wa kuwasaidia waathilika wa
mafuriko katika kijiji cha mwakata ambapo Wilayani Kahama yaliyotokea
hivi karibuni.Airtel imetoa msaada wa vitu mbali mbali kama vile sabuni
,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta.
Sehemu za Nyumba zilizoathiliwa na Mafuriko hayo.
Mmoja
wa waathirika wa Mafuriko huko Kahama,Bi. Helen Benjamin akiongea juu ya
hali halisi ya maafa hayo na kuomba serikali kuwapatia msaada.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua
katika wilaya ya kahama mkoani shinyanga kwa kuwapatia msaada wa
mahitaji muhimu yanayoitajika kwa sasa. Zaidi ya watu 35 walifariki na
kuwaacha mamia wakiwa hawana makazi ya kukaa kufatia mvua kubwa
iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu
Akionge
wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel Shinyanga
Bwana Ezekiel Nungwi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na
kutoa pole kwa familia zilizopoteza marafiki na wanafamilia kutokana na
mafuriko haya.
Tunatambua
pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao
kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja kutoa msaada
kwa namna tutakayoweza . Leo kwa niaba ya Ofisi yetu ya kanda ya
Shinyanga tunatoa msaada wa mabati, mablanketi, magodoro pamoja na
chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3 na kuwaomba watanzania
kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa kahama ili kuepuka milipuko ya
magonjwa isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida
mapema iwezekanavyo.
Sambamba
na mchango huu, tunapenda kuzindua namba maalumu itakayowawezesha
watanzania kuchangia. Tunachukua fulsa hii kuwaomba wateja wetu
kuchangia kwa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA kwenda namba 15626 , ujumbe
huu utalipiwa shiling 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko wa
kuchangia wahanga wa mafuriko mkoani Shinyanga,
Akiongea
kwa niaba ya wakazi wa Kahama helen Benjamin Alisema” Tunawashukuru
sana Airtel kwa msaada huu ulikuja wakati tunauhitaji zaidi,
Tunawashukuru kwa kuanzisha namba itakayowapa fulsa watanzania
kuchangia, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchagia na kwa
makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo
imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa
makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru
waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.