Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma
Athumani Kapuya akizungumza na watendaji wa Wakala wa Majengo
nchini (TBA) kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za Serikali, wakati
walipotembelea ofisi za Wakala jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akieleza jambo kwa Kamati ya Bunge
ya Miundombinu (hawapo pichani) kuhusuiana na mafanikio na
changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na hatua
zilizochukuliwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius
Mwakalinga akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Miundombinu, Prof. Juma Kapuya, wakati Kamati hiyo ilipotembelea
nyumba za watumishi wa Serikali eneo la Ada Estate jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius
Mwakalinga akiwaongoza wajumbe Kamati ya Bunge ya Miundombinu
kkwenda kukagua nyumba zinazojengwa kwa ajili ya watumishi wa Serikali
eneo la Mabwepande, Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Juma
Kapuya akipewa ufafanuzi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga, wakati Kamati hiyo ilipotembelea
nyumba za Serikali na kuona utekelezaji wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius
Mwakalinga akiwaonesha baadhi ya nyumba ambazo zinajengwa na TBA
(hazipo pichani)kwa ajili ya watumishi wa Serikali.
Baadhi ya nyumba za watumishi wa Serikali zinazojengwa na TBA eneo la
Mabwepande.