Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa kwa furaha na Mbunge wa
Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi
yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni
mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa
kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza
kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Lowassa amewafagilia Kinana na Nape kwa kazi nzuri wanaoifanya ya kuzunguka
mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama ambapo alimshauri Komredi
Kinana kupunguza kasi wanayokwenda nao kwani ni kubwa. Pia alisema hakuna katibu
wa chama aliyefanya kazi kubwa ya kukiimarisha chama kama Kinana.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa
Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi
yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni
mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa
kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na
kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mara
baada ya kuwasili Makuyuni,wilayani Monduli tayari kwa kuanza ziara ya siku 8
Arusha
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa
Jimbo la Monduli, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati wa mapokezi
yaliyofanyika Makuyuni, tayari kuanza ziara mkoani Arusha leo.ikiwa ni
mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa
kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza
kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizinduw mradi wa umeme vijini
(REA) katika kijiji cha Lolkisale,Wilayani Monduli mkoani Arusha
Baadhi ya Wananchi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana alipokuwa akiwahutubia katika kijiji cha Lolkisale,ambapo pia alizindua
mradi wa umeme vijijini (REA).
Pichani kulia,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la
Monduli,Edward Lowassa (kushoto) wakishiriki kupaka rangi jengo la hospitali ya
wilaya,jengo hilo hadi kukamilika zinatarajia kutumia kiasi cha fedha shilingi
bilioni tisa
Pichani kulia,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa jimbo la
Monduli,Edward Lowassa (kushoto) wakishiriki kuweka vitofali katika jengo la
hospitali ya wilaya,jengo hilo hadi kukamilika linatarajia kutumia kiasi cha
fedha shilingi bilioni tisa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa shangwe na wananchi
wa Monduli mjini
,Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi jengo la
kitega uchumi CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha
Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Monduli wakiwa wamejitokeza kwa wingi
kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana Monduli mjini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wakulima wa mpunga
wakishiriki kwa pamoja upaliliaji wa shamba la Mpunga,Mto wa Mbu,wilaya Monduli
mkoani Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwa sambamba na Mbunge wa
jimbo la Monduli,Edward Lowassa wakitoka kushiriki kupalilia shamba la
Mpunga,Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha.
Baadhi
ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo .
Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowassa akihutubia katika uwanja wa
barafu,Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Lowassa wakishangiliwa alipkuwa akihutubia katika mkutano huo
Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo