Baadhi
ya Maafisa, Askari na Mtumishi raia ambaye pia Mhasibu Mkuu wa Jeshi la
Magereza Estomih Hamis (Mzee wa Magereza Kileleni) wa saba kutoka
kushoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika
kilele cha Mlima Kilimanjaro asubuhi ya Machi 9, 2015 na kutundika
bendera ya Jeshi hilo kileleni.
Kiongozi
wa Msafara wa Maafisa, Askari na baadhi ya watumishi raia wa Jeshi la
Magereza waliopanda mlima Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza
Alexander Mmasy akiwa katika uso wa furaha mara alipowasili katika kituo
cha Gilman’s kabla ya kuanza safari ya kuelekea kilele cha Mlima huo
cha Uhuru. Kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Bakari Boi akiwa katika sura
ya uchovu baada ya safari ndefu ya usiku kucha kutoka Kituo cha Kibo
kuelekea Gilman’s.
Wakaguzi
wa Magereza Abas Mikidadi (katikati), Jamhuri Yassin (kushoto),
Deodatus Kazinja (aliyekaa kulia) na Bakari Boi wakiwa katika sura za
uchovu mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Gilman’s alfajiri ya
tarehe 09 Mach, 2015 baada ya safari ndefu na ngumu iliyoanza usiku wa
saa tano tarehe 08 Machi, 2015 kutoka Kibo kwenda Gilman’s kabla ya
kuhitimisha safari yao katika kilele cha Mlima huo cha Uhuru.
Baadhi
ya Maafisa, askari na watumishi raia wa Jeshi la Magereza na wasaidizi
wao (guiders) wakiwa wamepumzika usiku wa manane katikati ya njia ya
kutoka Kibo kuelelekea Gilman’s na baadae kilele cha Uhuru. Safari ya
kutoka Kibo kwenda Gilman’s ilianza usiku wa saa 5:13 Machi 8, 2015 na
kuhitimishwa Asubuhi ya saa moja Machi 9,2015.
Baadhi
ya Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakiwa katika nyuso za furaha
baada ya kuwasili katika Kituo cha Horombo kutoka Kituo cha Mandala
baada ya kutembea umbali wa kilometa 11 na kulala hapo kabla ya kuanza
safari ya kilometa tisa kutoka Horombo kwenda Kibo kesho yake.Kushoto
mwenye nguo nyeupe ni Kiongozi wa Msafara Kamishna Msaidizi wa Magereza
Alexander Mmasy na aliyeinua Mkono juu ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la
Magereza Estomih Hamis (Mzee wa Magereza Kileleni). Hamis ndiye
aliyekuwa na umri mkubwa kuliko wote katika kundi la watu 20 unaokaribia
kabisa miaka 60.
Kundi
la Maafisa, askari na watumishi raia wa Jeshi la Magereza pamoja wa
waongoza njia (guiders) kwa pamoja likiwa katika mwendo wa kilometa tisa
kutoka Horombo kwenda kituo cha Kibo ambapo liliwasili majira ya saa
tisa alasiri na kupumzika kabla ya kuanza safari ya kwenda Gilman’s saa
tano usiku.
Baadhi
ya Maafisa, askari na watumishi raia wa Jeshi la Magereza wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kuwasili katika kituo cha Mandala kutoka
Lango Kuu la Marangu. Mandala ni kituo kilicho umbali wa takribani
kilometa 8 kutoka Marangu na kiko katika mwinuko wa mita 2720 kutoka
usawa wa Bahari.
Mkuu
wa Gereza Kuu la Karanga Moshi Kamishna Msaidizi wa Magereza Dk. Hasan
Mkwiche akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi ya Mlima wa
Kilimanjaro Ndugu Erastus Lufungulo (wa kwanza kushoto) ikiwa ni ishara
ya kuwa amepanda Mlima Kilimanjaro na kufika kileleni. Dk. Mkwiche ni
miongoni wa Maafisa wa Magereza 16 waliofika katika kilele cha Mlima
Kilimanjaro cha Uhuru kwa upande wake ikiwa ni mara ya pili kupanda
mlima huo kwa mafanikio mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2011.
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza
Venant Kayombo akikabidhi bendera ya Jeshi la Magereza kwa kiongozi wa
Msafara wa wapanda mlima wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi wa
Magereza Alexander Mmasy katika Lango Kuu la Hifadhi ya Mlima Kilimanaro
kabla ya kuanza zoezi la kupanda mlima huo March 6, 2015. Picha zote na
Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja.
Kiongozi
wa Msafara wa Maafisa, Askari na baadhi ya watumishi raia wa Jeshi la
Magereza waliopanda mlima Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza
Alexander Mmasy (kushoto) akikabidhi bendera ya Jeshi la Magereza kwa
Mnadhimu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza
Dickson Mlay aliyemwakilisha Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro katika
kupokea msafara wa wapanda mlima wa Jeshi hilo katika Lango la Hifadhi
ya Mlima Kilimanjaro la Marangu.