Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akisalimiana na Kaimu Muuguzi Mkuu wa serikali Dkt.
Amalberga Kasangala mara baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya Kunduchi
Beach kufungua rasmi “The Scientific Conference for Lugina Africa
Midwives Research Network-LAMRN” tarehe 11.3.2015. Aliyesimama kushoto
kwa Mama Salma ni Ndugu Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
akifuatiwa na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baadhi
ya washiriki waliohudhuria mkutano wa Kwanza wa “Lugina Africa Midwives
Research Network” wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa kwenye mkutano huo.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na
viongozi kwenye meza kuu wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye
mkutano.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi tuzo Maalum kwa Bwana Maximillan
Lugina, iliyotolewa na wajumbe wa mkutano wa “Lugina Africa Midwives
Research Network” kwa ajili ya kumuenzi muasisi wa mtandao huo marehemu
Profesa Helen Lugina ambaye ni mkewe. Profesa Helen alikuwa ni Muuguzi
kutoka Tanzania aliyeasisi mkutano wa kwanza wa mtandao huo hapa nchini
mwaka 1992.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano wa kwanza wa “Lugina
Africa Midwives Research Network” uliofanyika katika Hoteli ya Kunduchi
Beach hapa Dr es Salaam tarehe 11.3.2015.
Wawakilishi
mbalimbali kutoka nchi za Africa wanaohudhuria mkutano wa kwanza wa
“Lugina Africa Midwives Research Network” wakimzawadia Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete mgolole mara baada ya kufungua rasmi mkutano huo huko
Kunduchi Beach Hotel tarehe 11.3.2015. PICHA NA JOHN LUKUWI