Mwandishi wetu
Taasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, (MISA) imemtangaza mrembo
mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo, kuwa miongoni mwa
wanawake tisa waliofanya mambo makubwa katika jamii kwa ukanda wa nchi
za Kusini mwa Afrika ijulikanayo kwa jina la “Misa’s Women to Watch’.
Kwa
mujibu wa taraifa iliyotolewa na MISA wakati wa siku ya wanawake
Duniani, Jokate ambaye ni mfanyabiashara, mwanamitindo, mtangazaji,
mwanamuziki, mbunifu wa mavazi na muigizaji wa filamu amepata nmafasi
hiyo kutokana na juhudi zake katika kuelimisha jamii na hasa afya ya
watoto na kuwawezesha wanawake.
Taarifa
hiyo imesema kuwa Jokate ambaye kwa sasa ana miaka 24, ameweza kuweka
msukumo mkubwa katika jamii mbali ya kujihusisha katika masuala ya
ujasiliamali kupitia nembo yake ya Kidoti.
“Ni
mfano wa wanawake walioamua kujiajiri pamoja na kuwa na elimu ya Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaam katika masuala ya Siasa, kwa umri wake mdogo,
ameweza kujihusisha na masuala ya afya ya mama na watoto na masuala ya
elimu,” ilisema taarifa hiyo.
Akizungumzia
hatua hiyo ya kutambulika, Jokate alisema kuwa utambuzi wake kutoka
Misa ni faraja kubwa na amepata amasa kubwa ya kuendelea na harakati
zake katika elimu, biashara, afya na kuwawezesha watoto wa kike.
“Nimeamua
kuitumikia jamii kutokana na vipaji vyangu, nashukuru kuona taasisi
kama Misa inanitambua na kuniweka katika kundi la wanawake tisa
waliofanya mambo makubwa katika jamii, hii inaonipa taswira kuwa kile
ninachokifanya kinajulikana na ndiyo lengo langu katika jamii,” alisema
Jokate.
Alifafanunua
kwa kusema kuwa taarifa hiyo imempa changamoto na kuwa mbunifu zaidi wa
nini cha kufanya katika maisha ya kila siku na hasa katika kujikwamua
kimaisha yeye binafsi na kwa jamii nzima.