Ofisa
mwakilishi wa Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Profesa Tolly Mbwette
akizungumza katika hafla maalumu ya uzinduzi wa awamu ya nne ya programu
hiyo jana Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
aizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo jana jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam.
Meza kuu katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.
Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues
(kulia) akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya
mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam.
Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam.
Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na
kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa
leo Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa toka meza kuu wakizungumza katika hafla ya uzinduzi
wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.[/caption]
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wamewezesha kozi kwa
baadhi ya nchi za Afrika yenye lengo la kuboresha mitaala ya elimu.
Akizungumza
kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela katika hafla
ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala, aliipongeza UNESCO
pamoja na taasisi zingine zilizounganisha nguvu kuhakikisha kozi hiyo ya
uboreshaji mitaala inafanyika.
Alisema njia pekee ya kuendelea kuboresha elimu yetu ni kutumia
wataalamu wa elimu hasa wanaohitimu katika kozi maalumu za ubunifu na
uandaaji mitaala kuiboresha mitaala hiyo kwa kuzingatia mahitaji halisi
taifa moja hadi lingine.
Alisema
awamu ya nne ya mafunzo hayo ya uboreshaji mitaala ambayo imezinduliwa
leo jijini Dar es Salaam na kujumuisha wanafunzi 100 kutoka nchi 23
ambazo ni pamoja na Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Zambia,
Swaziland, Niger, Senegal, Cameroon, Burkina Faso, Togo, Chad, Ivory
Coast, Nigeria, Hong Kong, Liberia, Sudan Kusini, Sierra Leone, Benin na
wenyeji Tanzania.
Aidha
Kilango katika hotuba yake ameiomba UNESCO pamoja na mashirika
wafadhili wa programu hiyo kuangalia uwezekano wa kuipanua zaidi na
kuboresha programu hiyo ili kuwa na manufaa zaidi jambo ambalo alisema
Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wowote kufaniisha jambo hilo.
Hata hivyo aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia nafasi walioipata
ipasavyo pamoja na kuifanyia kazi kitaaluma mara baada ya mafunzo hayo.
Alisema
elimu ya utaalamu wa mitaala ni muhimu kwa taifa lolote hivyo kutumia
utaalamu walioupata kuzishauri mamlaka kuboresha elimu kulingana na
maitaji.
UNESCO katika hafla hiyo iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues ambaye aliwataka wanafunzi watakao pata
mafunzo hayo kutumia elimu ya utaalamu ipasavyo ili kuboresha elimu.