Katibu
mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala
ya maendeleo ya jamii (CODERT), Hellen Kayanza akifafanua jambo wakati
wa shughuli iliyoandaliwa na Benki ya Exim jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki, kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo husherehekewa
Machi 8 kila mwaka.
Wakati
wa shughuli hiyo wafanyakazi wa kike wa benki hiyo walitoa wito kwa
wanawake nchini kutumia maadhimisho ya mwaka huu kutokomeza ukatili
dhidi ya wafanyakazi wa ndani. Wanaotizama ni Meneja mwandamizi wa
kitengo cha rasilimali watu wa benki ya Exim, Joan Mbakileki na Mkuu wa
matawi wa benki hiyo, Elizabeth Mayengoh.
Mkuu
wa matawi wa Benki ya Exim, Elizabeth Mayengoh (kulia), akikabidhi
zawadi kwa Katibu mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali
inayojishughulisha na masuala ya maendeleo ya jamii (CODERT), Hellen
Kayanza (wa pili kulia) wakati wa shughuli iliyoandaliwa na Benki ya
Exim jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha siku ya wanawake
duniani ambayo husherehekewa Machi 8.
Wakati
wa shughuli hiyo wafanyakazi wa kike wa benki hiyo walitoa wito kwa
wanawake nchini kutumia siku hiyo kutokomeza ukatili dhidi ya
wafanyakazi wa ndani. Wanaotizama ni Mkuu wa matawi wa benki hiyo, Agnes
Kaganda (kushoto) na Meneja mwandamizi wa kitengo cha rasilimali watu
wa benki ya Exim, Joan Mbakileki.