Akiongea na waandishi wa habari leo,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema anawaomba watanzania wote wanaotaka kuchangia wahanga hao kutuma fedha zao kwenye namba maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.
“Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole waathirika wote na tunaungana na wakazi wa kahama kwa janga hili tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia kitengo chetu cha kusaidia jamii cha Vodacom Foundation na tunawaomba watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.
Alisema kupitia njia hii ya namba maalumu ya”Red Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi ya uchangiaji.
Jinsi ya kuchangia ni rahisi sana unachotakiwa kufanya unaponyeza *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.