![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_umyvNuVMXokVSuG7TJ63_5hVjDp5a6-Mn8Z3f9tlwtPKcBtrV7CE5KOWVcnV30bf4z7oBCqfdsiv187cChKJ_OvL9UvWPBxKMVgiNdgr1HjYDML96G67V0abjTYRFXn4CBWVelLN7B74g23-8XUkmEOrE6OXw4nlJoF4QlEmHwi-LLkM2Sor6DAyllnRUbx4xBIKR12H78_5pu5qR-Wb2A7FmGV20cnpyYhOY8WRUdoFXoBXlhyio=s0-d)
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wa Dar es Salaam (JWT), Philimon Chonde
akizungumza katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge
uliofanyika Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vIjJNEhoczKC5wjBzHHoTTivITUEf8rUpDETg2fb_1OekbJxPXdSH70FRRJCkZfuPSKtonQoZk7KIlBx4r5cWWM5GVhs39Jz-0HtWJ0_zPUZhpkQ1WaIfhfnVB9WqICxeUrabXP4r-GdvHDp-yCAhspexMCqARnv33uZV-tAKvoZbOEo-6r6GsP5GRHZL32PO7PlaNggf1ln0nCVY4DQYIfjMX5wE_jRI2t5WMkRnZMeNDClTv_Z8=s0-d)
Mbunge
wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu akisisistiza jambo katika mkutano wa
Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika Machi 5, 2015 Ukumbi
wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vRypLtpwfSZ9rtBHY-18p5IV5BmJ3MWVrsWAWLJJaEWskzP_88cA65hzSn9PaKM-VaAoWqBZokc8qVJNk1cDL3V5zhWPVAZQeMtXuoEubyYkO589UebGws1QQckVyb-y0XlAbjTwmCqGupEZMiqu5KnbmcveIn8TJwpjKNJZz2lOFM2ZOgnT_n29HFJVGVnwbsIkkjF71Q5g-iY1huy_iErJbIWMnY652cAOfUkSO0nrXbshEcoHs=s0-d)
Mbunge
wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akifanya majumuisho katika mkutano wa
Wafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika Machi 5, 2015 Ukumbi wa
Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vLp_sFRd0mVg9tnM3kqjVgV_e7WJ4Nye6r1c53GmUGRBWg2x3LpTd55jfXBQt9HC1XFCWGvkx2JdZqsnJQjzyaBSXU0d70DoFB1OVz1yHQpiZyT7Nqxmuo8xAib69H-WA1eGvcLQggLzmtyTH-RLNo6332dihPpBxNxuF8qk5_3O3EO0DjtO1JnDUXvg9kJzuQ9W1rDhvEVgQrVH_OFTXFxp2MQxnfOjmm1-Uz0CJxeyx0elEtVwSZ=s0-d)
Mmoja wa wafanyabiashara akiombea mkutano kabla haujaanza.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_updTvGYoVij_2C8uAhWqqsYStIiR7vkbFn-PN7JAUaRnH7LmbnvEkGIvDTa5bShy9rdAFPw1TM1snV_lUJpDoLCFgLOZZejgJebRuK_W0y3_hbbtpbwwa0ERZbkgW8qoWDN7u4a16Q81Dteodtfo3ptAW47924YNPn0NbwgyriYu7cLJyKlITL7vTmTWaV2WC6yeSGzqa-NU-d0j6CL_TjqjLLldB6mkjYKIA7FITaZLuWewx0qrP4=s0-d)
Mbunge
wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akisalimia na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa
Azan Zungu katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge
uliofanyika Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vCS6gcmYr074iShEsbD7gK2jdBWRhAILH7QoO0VJWrnwpqtmrrYP0O_RKdcr7hRH_Vk7JtJVeA33lIWZhY6jB8mHUaI2cfiYrbD1u3i0hhx_5S-amhv2qURYF6t__9XFfzggd-XoW0tbFLWuSSkdo23H1RjPqQBQM6kaRp_JVtmrdzAEGq_z3hPDGmK7eCwQ5o0-b0tMyMDhmMW4W8KnLXupikIzjuD8lHJ9mXrZ_rhfzRObBGfKTS=s0-d)
Waheshimiwa
wabunge wa jiji la Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mkutano,
kutoka kulia ni Mhe. Abbas Mtemvu, Mhe. John Mnyika na Mhe, Mussa Azan
Zungu.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_tUSlVvciIfBcxjrSq3Kj3QmZXAEm9bVQTr6BMKxf_XLV0J5pEqeMAZylhM9F7wepxMQ_KuEkE3pQVZ6xKbM2CBzBgD4pwEKqWVaLi4wIinu5PQKzsyjAumh0R1Grj9GyRtPH0gMd8GODRDtH7PpjXh1Vc8Rf4iz4wDsasnXtJK5lv2kd2doU5bdALnwSqxGcgzIqEypqM_r5xnT5y9ppkETFd3keWpc7VisGp0d0L-toNZEvWt7M0=s0-d)
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Dar es salaam (JWT), Philimon
Chonde amesema suala la kupandishwa kwa kodi kwa asilimia mia moja
limepitishwa kinyemela bila ya wao kuwashirikisha wala kujadiliana na
wafanyabiashara hao.
Akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Lamada
Hotel jijini Dar es Salaam ukiwashirikisha wabunge, ameeleza kuwa mfumo
wa kodi uliopo umekaa kikoloni kwani unawakandamiza wafanyabiashara ili
waendelee kuwa tawala kwani haungalii uwiano uliopo baina ya
wafanyabiashara wakubwa na wafanyabishara wadogo.
Chonde amesema kutokana na kuwepo kwa usumbufu wa kudai leseni
ameitaka Serikali kuweka suala la kodi katika mfumo unaoeleweka ili
kumsaidia mfanyabiashara kujua ni kiasi gani anatakiwa kulipa kwa mwezi.
Naye Mbunge wa Temeke Abasi Mtevu amezitaja changamoto zinazowakabili
wafanyabiashara hao ni suala la usafi wanalipia lakini mazingira bado
ni machafu na wamesema wapo tayari kufanya usafi wenyewe na suala la
zima moto kwamba kila mfanyabiashara aweze kuwa na mtungi wa gesi lakini
hawapewi mitungi hiyo bali hupewa karatasi ya malipo.
Pia amesema sheria zinazopitishwa Bungeni baadhi ni kweli na nyingine
zimetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi na amewasisitiza
wafanyabiashara kupambana katika kulinda biashara pamoja na mitaji yao.