Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akitoa maelezo ya hali ya migogoro
ya Ardhi iliyopo Mkoani Mwanza kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi alipokutana na Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa katika ziara yake Mkoani Mwanza.Picha na Muungano
Saguya- Mwanza
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mh. Jaji Mfawidhi Makalamba alipokutana
naye ofisini kwa Jaji huyo Jijini Mwanza ili kupata namna bora ambayo
mhimili wa mahakama unaweza kusaidia kutatua migogoro ya ardhi nchini.
Waziri Lukuvi yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Mwanza yenye nia ya
kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Jijini Mwanza
Mh. Makaramba na watendaji wa sekta ya ardhi na mahakama alipomaliza
mazungumzo na Jaji huyo jana.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akisiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi kanda ya ziwa
Bw.James Silas (hayupo pichani) alipotembelea Baraza hilo jana kuona
namna wanavyoshughulikia mashauri ya ardhi na kutoa haki kwa wananchi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akimkabidhi Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi kanda ya ziwa Bw.James
Silasshilingi milioni moja(1000,000/=) ili kununua karatasi za kuwezesha
utoaji wa hukumu za wananchi zinazohusu kesi za ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akiwasalimia Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela alipowasili
katika Halmashauri hiyo kukagua shughuli za ardhi na kusiliza moja kwa
moja malalamiko ya wananchi na kutatua kero zao.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akikagua utendaji wa watumishi wa Mipango Miji na Ardhi Wilayani
Ilemela. Katika ukaguzi wa ghafla alioufanya katika masijala hiyo,
Waziri Lukuvi aligundua mafaili kutofanyiwa kazi ipasavyo na watendaji
hao hivyo kuwafanya baadhi ya wananchi kutopata haki zao kwa mika
takribani 21.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akitoa maelezo ya awali kwa wananchi wa Wilaya ya Ilemela (hawapo
pichani) waliofika kueleza kero zao. Katika mkutano huo Waziri
alisisitiza Maafisa Ardhi na Mipango Miji kufanya kazi kwa kufuata
maadili na haki ili kuwaondolea wananchi wanyonge kero za ardhi.
Mmoja
wa wananchi takribani 60 waliofika na kuwasilisha malalamiko ya kunyimwa
haki ya ardhi na watendaji wa ardhi na mipango miji Wilayani Ilemela
kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian
Vangimembe Lukuvi jana.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi
akipokea rundo la malalamiko ya wananchikutoka kwa Wenyeviti wa Mitaa
yahusuyo ardhi alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Mwanza
jana. Waziri Lukuvi kesho atakutana na wananchi wengine katika
Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kusikiliza kero zao.