MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Apr 14, 2015

HILI NDIO TATIZO LINALOWAKABILI MASTAA WA FILAMU TANZANIA { BONGO MOVIES }

Mastaa Bongo Movie Njaa Tupu!
Uchunguzi uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba mastaa wengi wa sinema za Kibongo wapo katika hali ngumu kiuchumi kutokana na soko la filamu kudorora huku wizi wa kazi zao na kusitishwa mikataba yao na makampuni makubwa ya usambazaji vikichangia.

Uchunguzi huo umebaini kwamba moja ya makampuni yaliyositisha mikataba ya wasanii ni Steps Entertainment ambao wamesababisha mastaa kibao kushindwa kutengeneza muvi kwa kuwa awali walikuwa wakipewa bajeti na Steps kisha kuwauzia kwa bei ya mapatano.
Ilibainika kwamba baada ya Steps kuachana na utaratibu huo na kudai kuwa wanachukua muvi zilizoandaliwa na makampuni binafsi za mastaa wachache kama Jacob Steven ‘JB’, Athuman Amri ‘Mzee Majuto’, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine wenye makampuni binafsi.
Mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu, Musa Issa ‘Cloud 112’ alikiri kuwepo kwa hali hiyo huku akifafanua kuwa Steps kuna wakati inakuwa kwenye kipindi kigumu.
Wewe kama mdau una maoni gani juu ya hili.