Uchunguzi wa chembechembe za DNA
unatarajiwa kufanyiwa kile maafisa nchini Iraq wanasema kuwa ni mwili wa
Izzat Ibrahim al Douri ambaye ni mwanachama wa mwisho wa uliokuwa
utawala wa Saddam Hussein ambaye amekuwa akitafutwa.
Maafisa wa jeshi wanasema kuwa aliuawa na vikosi vya serikali wakati msafara wake uliposhambuliwa karibu na mji wa TikritBwana al Douri anaaminika kuchangia pakubwa katika ukuaji wa kundi la Islamic State nchini Iraq.
Aliyekuwa msemaji wa chama cha Baath ambacho kilikuwa chama chake al - Douri alikana kuuawa kwake.
bbc