Wavuvi
wakirejea pwani baada ya shughuli ya kuvua samaki. Inaelezwa kwamba
wavuvi wadogo kama hawa wakiwezeshwa siyo tu wanajiongezea kipato chao
lakini pia inawasidia katika utunzaji wa mazingira ya bahari .
Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
akizungumza wakati wa mkutano wapembezoni kuhusu masuala ya uvuvi
endelevu, katika mchango wake, Balozi ameeleza kuridhwa kwa Tanzania
namna ambavyo wadau mbalimbali wamekuji wakijitokeza kusaidia sekta ya
uvuvi na wavuvi nchini Tanzania
Balozi
Manongi akibadilishna mawazo na Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni mtaalamu
wa masuala ya utaifiti na ambaye alieleza kwamba Norway iko katika
maandalizi ya mwisho ya kukamilisha meli mpya na ya kisasa zaidi ya
utafiti itakayoanza kazi mwakani.
Hapa
Balozi akibadilishana mawazo na Dr. Gabriella Bianchi ambaye pia ni
mtaalamu wa masuala ya utafiti wa samaki, Dr Gabriella na Dr, Hoel
wamefanya kazi kwa karibu sana na wataalamu wa Tanzania katika
kuendeleza sekta ya uvuvi.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wa pembezoni
Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania,
kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi
Tuvako Manongi, imeelezea kuridhishwa kwake na namna ambavyo
Mashirika ya Kimataifa naTaasisi binafsi zinavyoshirikiana na kwa
karibu na serikali na taasisi zake kuimarisha sekta ya uvuvi.
Ushirikiano
huo umeifanya sekta ya uvuvi nchini kuwa wenye tija na hivyo kuchangia
katika ongezeko la kupato na kuwaondoa katika umaskini jamii ya
watanzania ambao maisha yao ya kila siku yanategemea sana uvuvi, na pia
kuimarisha utuzaji wa mazingira ya pwani na viumbe hai.
Balozi
Tuvako Manongi ameyasema hayo wakati wa mkutano wa pembezoni ( side
event) uliokuwa umeandaliwa na Mpango wa Chakula Dunia ( FAO). Mkutano
huo umefanyika sambamba na mkutano usio rasmi ambapo nchi wanachama wa
Umoja wa Mataifa, wakutana ana kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya
bahari na uwiano wake katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo
Endelevu baada ya 2015.
Balozi
Manongi alikuwa mmoja wa wazungumzaji katika mkutano huo ambapo
majadiliano yalilenga zaidi katika suala zima la uwezeshwaji wa
wataalamu wa sekta ya uvuvi na wavuvi wadogo na wakati kwa kuwapatia
mbinu na maarifa ya kisasa ya uvuvi endelevu na unaozigatia utuzaji wa
mazingira ya bahari na viumbe hai.
Katika
mchango wake, Balozi ameeleza kuwa uchumi na ustawi wa wavuvi wengi
wanaoishi pembezoni mwa bahari (pwani) nchini tanzania unategemea sana
shughuli za uvuvi na kutoka na ukweli huo, Serikali ya Tanzania,
licha ya kukaribisha wabia katika kuiendeleza sekta ya uvivu pia
inawashukuru wale wote ambao hadi sasa wametoa mchango wao wa hali na
mali katika eneo hilo.
Akaongeza kuwa mafunzo na utaalamu ambao wadau hao wamekuwa wakiwapatia
wataalam wa kitanzania kwa kuwashirikisha pia wavuvi ambao ndio
wahusika wakuu, umesaidia sana katika kuwainua kiuchumi lakini pia
kuwapatia mbinu endelevu za uvuvi na utunzaji wa mazingira.
Wadau
ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo endelevu ya
sekta ya Uvuvi ikiwamo misaada ya kiufundi ni FAO na EAF- Nansen
Project ya Norway.
Tanzania ni kati ya nchi 32 ambazo zinashirikiana kwa karibu na EAF
–Nansen Project katika miradi mbalimbali inayohusu uwezeshwaji wa
wavuvi wadogo na wakati.
Aidha
Tanzania ni kati ya nchi 10 za mwanzo zilizochaguliwa kutekeleza
mpango huo.
Amesema Balozi Manongi, uvuvi endelevu na matumizi salama ya Bahari
ni moja ya ajenda za Malengo Mpya ya Maendeleo Endelevu baada ya
2015 (SDGs).
Ajenda
ambayo kwayo inasisitiza usimamizi endelevu na ulinzi wa bahari
na mazingira ya pwani na viumbe hai ili kuepusha athari mbalibmali.
Vile vile ajenda hiyo ambayo ni namba 14 inasisitiza pia uwepo kwa
kanuni bora zinazosimamia uvuvi ikiwa ni pamoja na kudhibiti uvuvi wa
kupita kiasi na uvuvi haramu, na utoaji wa huduma za kisasa kwa wavuvi
wadogo na fursa za masoko.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa ameeleza zaidi kwamba,
zao la samaki pamoja na kuwa kuchanzo cha kipato kwa watanzania
wengine na taifa kwa ujumla, lakini pia samaki wanachangia katika
kuwapatia lishe bora watanzania na kwa sababu hiyo matumizi endelevu
ya mazao ya bahari na bahari ni jambo muhimu sana.
Katika
majadiliano hayo, Dr. Gabriella Bianchi ambaye ni mtaalamu wa masuala
ya utafiti wa samaki kutoka ofisi za FAO yeye katika mchango wake,
ameelezea baadhi ya mambo ambayo wanatarajia kuyafanya katika
kuzisaidia nchi za Afrika Mashariki Tanzania ikiwamo na kwingineko
Afrika katika masuala ya usimamizi, mafunzo na utaalamu zaidi
kwenye masuala ya samaki na bahari kwa ujumla.
Akasema
mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za utafutaji na uchimbaji wa mafuta
na gesi, na uchafuzi wa bahari ni baadhi ya changamoto ambazo
wataalamu na watafiri wa masuala ya bahari na viumbe hai wa baharini
kuamua kupanua wigo wa kazi zao za utafiti ikiwa ni pamoja na mafunzo
na uwezeshaji.
Naye
Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya utafiti, amesema
Norway inakamilisha ujenzi wa meli mpya na ya kisasa ya masuala ya
utafiti inayotarajia kuanza shughuli zake mwaka 2016.
Kwa mujibu wa Dr. Hoel meli hiyo itakuwa na vyumba vya kufundishia, maabara za picha na maabara ya tabia nchi
habari kwa hisani ya michuzi media