Ofisi
ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada kwa ushirikiano na The Canadian
Comprehensive Auditing Foundation - La Fondation Canadienne Pour la
Verification Integree (CCAF - FCVI Inc.), kwa pamoja wameandaa hafla ya
kutangaza vivutio vya utalii vya nchi za Tanzania, Senegal na Ghana.
Hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada pia imedhaminiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada.
Katika
hafla hiyo ambayo iliambatana na utoaji wa mada juu ya utamaduni na
utalii, Tanzania iliwakilishwa na Bi. Ndyanao Mgweno na Bwana Andrew
Kellei ambao wanatoka katika Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali wa Tanzania.
Maafisa
hao wako nchini Canada kwa mafunzo ya Ukaguzi wa ufanisi (performance
Audit) ambayo yanatolewa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Canada.
Shughuli za kutangaza utamaduni wa Utalii wa Tanzania ilisimamiwa na
Ubalozi wa Tanzania nchini Canada ambapo Mheshimiwa Balozi wetu huko
Canada Mhe. Jack Zoka aliwakilishwa na Kaimu wa Kitengo cha Utalii na
Mwambata wa Fedha wa Ubalozi huo Ndg. Richard Masalu.
Banda la Tanzania limetia fora kwa vielelezo na vivutio vya utalii kati ya mabanda mengine kama inavyoonekana katika picha.