Foleni
ya Wakimbizi kutoka Burundi kuelekea kwenye mabasi maalum
yaliyoandaliwa na Shirika la IOM kuwapeleka kwenye eneo maalum la kambi
ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushoto)
pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa
Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa
pili kulia), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kulia) mara
tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma,
eneo ambalo Wakimbizi wanapokelewa na kupewa huduma ya kwanza kabla ya
kuelekea katika eneo maalum ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mh.
Chikawe akizungumza na wafanyakazi wa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
wanaoandikisha Wakimbizi wanaowasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika
kabla ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Amah
Assiama-Hillgartner (kushoto) akifafanua jambo kwa Alvaro Rodriguez (wa
tatu kushoto) pamoja na Joyce Mends-Cole (wa pili kushoto)
walipotembelea uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Mmoja
wa watoa huduma kwenye kituo cha muda cha Wakimbizi katika viwanja vya
Lake Tanganyika akipuliza dawa ya kuua wadudu kwenye mifereji
inayozunguka uwanja huo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya
milipuko ikiwemo Kipindupindu.
Mh.
Chikawe (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya Wakimbizi kutoka
Burundi waliokuwa kwenye foleni ya kupanda mabasi kuelekea kambi ya
Nyarugusu kwenye makazi maalum yaliyotengwa na Serikali ya Tanzania
yanayohudumiwa na Shirika linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika
mengi ya Umoja wa mataifa.
Alvaro
Rodriguez (kulia), Mh. Chikawe (wa pili kulia) pamoja na Joyce
Mends-Cole wakishuhudia baadhi ya Wakimbizi wakipanda mabasi maalum
yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la IOM tayari kuelekea
katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
...Zoezi likiendelea.
...wakiendelea kupanda kwenye mabasi.
Alvaro
Rodriguez (aliyeipa mgongo kamera kushoto), Mh. Chikawe (wa pili
kushoto) pamoja na Joyce Mends-Cole wakiagana na baadhi ya Wakimbizi
wanaoelekea kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma
kutokea katika kituo cha muda cha mapokezi na huduma za afya kilichopo
katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Baadhi
ya wakina mama na watoto zao wakiwa wamejipumzisha ndani ya viwanja vya
Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya
Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Wahudumu
wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wakiwapulizia dawa maalum
kwenye mikono na miguu kwa ajili ya kuua bakteria kabla ya kuingia ndani
ya mabasi na kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
...zoezi likiendelea.
...wakiendelea kupuliziwa dawa maalum ya kuua bakteria.
Mh.
Chikawe akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Alvaro Rodriguez (kushoto) wakielekea kutembelea mabanda
mbalimbali ya huduma za afya yaliyopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika
yanayotoa huduma kwa Wakimbizi wanaowasili kabla ya kupekwa kambini.
Baadhi
ya watoto wakipatiwa matibabu ndani ya kituo cha muda kabla ya kuelekea
kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Wazazi na watoto wakiwa kwenye hema maalum, huku nwengine wakiwa kwenye dripu za kuongezewa maji mwilini.
...wagonjwa waliolazwa wodini.
Wafanyakazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wakisafisha
mikono yao na kupuliziwa dawa maalum katika viatu mara baada ya
kutembelea mahema yenye wagonjwa mbalimbali Wakimbizi kutoka Burundi
wanaopatiwa matibabu kwenye kituo cha muda kilichopo kwenye viwanja vya
Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Baadhi
ya watoto wakijiliwa na kujifaraji kwa kucheza mpira katika kituo
maalum cha kupokelea Wakimbi wanaotafuta hifadhi nchini Tanzania
wakitokea nchini Burundi katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Familia
za Wakimbi wakiwa wamejipumzisha kwenye kituo cha muda katika viwanja
vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya
Nyarugusi iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
...wakiwa wamepumzika.
Sehemu ya eneo la uwanja wa Lake Tanganyika.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katikati ya
wiki wametembelea eneo la mapokezi ya Wakimbizi kutoka Burundi lililopo
katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.Walipofika katika eneo hilo la mapokezi waliojionea huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula duniani (WFP), Shirika la afya duniani (WHO) pamoja na Shirika la UNFPA linaloshughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Wakimbizi wengi waliofika eneo hilo walikuwa na afya dhoofu kutokana na kusafiri kwa umbali mrefu.
Kutokana na hali hiyo baadhi yao ilibidi wapatiwe huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya makazi yaliyotengwa kwa Wakimbizi ikiwemo kambi ya Nyarugusu iliyopo katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Hata hivyo kambi hiyo ya Nyarugusu ina uwezo wa kuchukua sio zaidi ya Wakimbizi 50,000 lakini sasa ina Wakimbizi zaidi ya 48,000 kutoka Burundi na 60,000 kutoka Jamuhuri ya watu wa Congo.
Aidha Waziri Chikawe alisema kuwa Serikali imetenga eneo maalum ambalo litajengwa kambi mpya itakayojulikana kama Nyarugusu B ambayo itakuwa ni mahususi kwa Wakimbizi kutoka Burundi.
Mh. Chikawe alisema kuwa kambi hiyo itakamilika ndani ya miezi mitatu kutoka hivi sasa, ili kuwatenganisha Wakimbizi kutoka Congo na Burundi.
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewji Blog)