Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi
wa habari jioni hii juu ya kilichofanyika kwenye Mkutano wa Halmashauri
Kuu ya CCM, ambapo amesema kuwa sasa NEC inapiga kura kupata majina
matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika Usiku
wa leo majira ya saa tatu, kwenye Ukumbi wa Dodoma Convetion Centre.