Vipeperushi hivyo vinasema uteuzi wagombea
urais ndani ya CCM umekuwa ukigubikwa na mizengwa kwa muda mrefu sasa,
na kwamba wagombea wasiokubalika ndiyo wanaoteuliwa huku wanaokubalika
na wananchi wakiachwa ili kulinda maslahi ya watawala wanaomaliza muada
wao.
04:45 Kikao cha Halmashauri Kuu bado
kinaendelea, taarifa zilizotufikia muda sio mrefu zinasema kuwa
inaonesha mvutano ni mkali kuhusu kuchagua majina matatu ambayo
yatapelekwa kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuyapigia kura lipatikane
moja.
Taarifa zinasema kutokana na mvutano huo, muda wa Mkutano Mkuu itabidi usogezwe mbele. Ulitarajiwa kuanza saa nane mchana
14:13 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM
umeanza saa chache zilizopita, baadhi ya wajumbe wamempokea Mwenyekiti
wa chama hicho, Jakaya Kikwete kwa nyimbo kuwa wana imani na Lowassa.
Kikwete awatuliza wajumbe hao kisha afungua kikao na kuanza kusoma ajenda za kikao hicho.
Taarifa zaidi kuhusu kikao hicho edelea kuwa nasi
11:50 Mheshimiwa Edward Lowassa amezungumza
kwa ufupi na Wanahabari kuhusu jina lake kukatwa, Lowassa amesema
hajasikia taarifa hizo na kuahidi kuwa akipata taarifa hizo atazungumza.
10:27 Katibu wa Itikadi na Uenezi azungumza na
waandishi wa habari mjini Dodoma, awaambia kuwa hana sababu ya kuyataja
majina yaliyotoka kamati kuu kwa sababu tayari yameshajulikana
1:32 Tovuti ya CCM imeyatangaza majina matano
yaliyopitishwa na Kamati ya CCM (CC) kuwa ni Bernard Membe, John
Magufuli, Asha-Rose Migiro, January Makamba na Amina S Ali
12:55 Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CC) kimemalizika hivi punde mjini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Ueneze
Nape Nnauye ameshindwa kutaja majina matano ambayo yatapelekwa kwenye
Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC)
Badala yake amewaambia waandishi wa habari kuwa majina hayo yatatangazwa saa nne asubuhi.
Aidha kwa mujibu wa Matangazo yaliyorushwa moja kwa moja na
kituo cha redio Uhuru, Sophia Simba alisikika akisema kuwa mvutano mkali
ulikuwemo ndani kikao hicho na wajumbe, Adam Kimbisa, Dk Emmanuel
Nchimbi na yeye mwenyewe hawakukubaliana na maamuzi ya kikao
yaliyofikiwa.
10:10 Bado kikao cha Kamati Kuu (CC) kinaendelea
taarifa zilizopo ni kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
kimeahirishwa hadi kesho saa nne asubuhi
8:12 Kikao cha Kamati Kuu kinarudi kuendelea na
kitatoa taarifa ya majina matano ambayo kwa sababu ya muda yatajadiliwa
kesho na Kikao cha Halmashauri na Mkutano Mkuu utafanyika kesho mchana,
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
7:00 Kamati Kuu ya CCM imeeenda mapumziko mafupi kwa ajili ya Kufuturu na watarejea tena majira ya saa mbili usiku.
4:30 KUMEKUCHA Dodoma, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mkutano wake wa Kamati Kuu saa chache zilizopita.
Taarifa kutoka Dodoma zinasema watu wote
wameondolewa ndani ukumbi mpya wa CCM ikiwa ni pamoja na waandishi wa
habari ambapo hivi sasa wanasubiri taarifa hizo nje ya ukumbi huo.
Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi kutoka Dodoma ......
chanzo: Mwananchi
chanzo: Mwananchi