MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Aug 2, 2015

AIRTEL FURSA YAWEZESHA VIJANA ZAIDI YA 200 ARUSHA MBINU ZA KUENDESHA BIASHARA ZAO

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika jijini Arusha jana.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha, Blandina Nkini akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika jijini Arusha jana.

Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika jijini Arusha jana.
Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika jijini Arusha jana.
Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Gema Kavishe (wa pili kushoto), akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika jijini Arusha jana.

Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia mtaji wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”* imeendesha semina ya mafunzo ya biashara kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kutoa ujuzi na mbinu za kumbambana na changamoto za biashara na jinsi ya kuendesha biashara zao katika ukumbi wa Golden Rose Mjini Arusha.
Vijana wengi waliweza kuhudhuria semina hiyo ambayo iliwapo mafunzo ambayo yataweza kuwasiadia katika kutatua changamoto wanazokutana nazo katika maisha yao ya kila siku na katika ulimwengu wa sasa wenye ushindani mkubwa wa biashara.
Airtel, Kupitia mradi wake wa *Airtel Fursa “Tunakuwezesha”* umewawezesha vijana zaidi ya mia mbili kupata mafunzo ya biashara na pia wengine kubahatika kwa kuwezeshwa na vitendea kazi vya kuinua biashara zao. Mikoa ambayo imeweza kuwezeshwa mpaka sasa ni Dar Es Salaam, Mwanza na Arusha na wiki ijayo wakaai wa Mtwara watawezeshwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya alisema “Tunajivunia kudhamini semina hii kwa kuwa moja ya dhamira ya kampuni yetu ni kuwawezesha vijana hapa nchini kwa namna mbalimbali ikiwemo
kuwapatia maarifa na ujuzi kama ambavyo katika semina hii wameweza kupata mbinu za kuendesha biashara zao na tunaamini wakizitumia wataweza kupata mafanikio na maisha yao kuwa murua.”
Aliongeza kuwa Tanzania kama zilivyo nchi nyingine imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ajira hususani kwa vijana. Kukosa mbinu za kupata mikopo, na ushindani mkubwa uliopo kwenye soko la biashara.”Mafunzo haya ni muhimu na yanaenda sambamba na utekelezaji wa malengo ya kuwainua wajasiriamali ili kuweza kuwainua vijana hapa nchini,” alisema.
Baadhi ya vijana waliohudhuria semina hiyo waliishukuru Airtel kwa kuandaa semina ya kutoa ujuzi wa baishara katika nyanja mbalimbali.
”Tumeweza kupata maarifa na tunawashukuru sana Airtel kwa kufanikisha kuwepo semina hii. Kuna vijana wengi sana huko mtaani ambao hawajui pakuanzia ili kupata elimu ya kuinua biashara zao. Lakini leo hii, Airtel imeona umuhimu wetu na kuamua kutuwezesha kwa kutupatia mafunzo haya muhimu,” alisema Bi Naima Aboubakar mmoja wa washiriki kwa niaba ya wenzake