New York, Marekani
MWANAMITINDO, Amber Rose hivi karibuni amefanya kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kulipa kisasi kwa mwanamitindo mwenzake, Kim Kardashian cha kummiliki x-boyfriend wake, Kanye West baada ya kuonekana usiku wa manane na aliyekuwa mume wa Kim, 6+99 Kris Humphries.

Chanzo kinafunguka kuwa tukio hilo lilijiri kwenye ukumbi wa usiku wa Playboy Mashion. “Amber hakufurahishwa na kitendo cha Kim kutoka na x-boyfriend wake ndiyo maana ameamua kuwa karibu kila kona na Kris ili alipe kisasi,” kilisema chanzo.
Kim na Kris waliwahi kufunga ndoa mwaka 2011 iliyodumu kwa muda wa siku 72 kisha kuachana ambapo miezi sita baadaye aliingia kwenye uhusiano na mumewe wa sasa, Kanye West ambaye naye kabla alikuwa kwenye uhusiano na Amber Rose tangu mwaka 2008 uliodumu kwa miaka miwili.