MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Aug 6, 2015

AIRTEL YAZINDUA MNARA NYAKASUNGWA SENGEREMA, MWANZA NA GEITA


Afisa Elimu wa Wilaya ya Sengerema Benjamin Sipetro akikata utepe kuzindua mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel katika kijiji cha Nyakasungwa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wa tatu kulia ni Meneja masoko kanda ya ziwa Emmamuel Rafael.

Afisa Elimu wa Wilaya ya Sengerema Benjamin Sipetro AKIKABIDHI VITABU VYA MASOMO YA SAYANSI katika shule ya sekondari ya Nyakasungwa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza,wa tatu kulia ni Meneja masoko kanda ya ziwa Emmamuel Rafael.
Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyakasungwa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wakifurahia vitavu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na kampuni ya Airtel kuunga mkono juhudi za serikali kutaka wanafunzi wasome masomo ya sayansi.
Kukosekana kwa mawasiliano ya uhakika maeneo ya vijijini inaelezwa kuwa ni kikwazo kwa wakulima kushindwa kujua hali ya soko na kujikuta wakiuza mazao yao kwa bei ya chini na hivyo kushindwa kufikia malengo ya kujikwamua na lindi la umasikini.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema aliyewakilishwa na Afisa Elimu Sekondari Benjamini Sipetro ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Nyakasungwa wilaya Sengerema mkoani Mwanza utakaohudunia zaidi ya vijiji saba Sipetro amesema wakulima wengi mazao yao yanaozea shambani kutokana na kukosekana kwa mawasilaino ya uhakika "Ndugu zangu ninaamini mawasiliano ya uhakika yatamfanya mkulima kutumia teknolojia inayomzunguka kufanya biashara na kupata masoko ya mazao yao na malipo kupitia huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo huduma ya Airtel Money.
Napenda kutoa wito kwa wakazi wa kijiji hiki cha Nyakasungwa na vijiji jirani kutumia vyema mawasiliano haya na kuleta ufanisi katika shughuli zao za kijamiina kiuchumi. Tunawashukuru sana Airtel kwa kutufika na kutatua changamoto sugu ya mawasiliano tuliyokuwa nayo hapo awali.
Aliongeza Sipatro Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni ya Airtel Kanda ya ziwa Emmanuel Raphael alisema" Tunajisikia furaha kusogeza huduma za mawasiliano ya simu ya uhakika kwa wakazi wa Sengerema na Geita.
Tunaamini kwa kupitia mawasiliano haya tutaleta chachu ya maendeleo kwa wakazi walioko hususani katika maeneo ya pembezoni mwa nchi na Tanzania kwa ujumla."Wakati huo Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie amekabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi kwa shule ya Sekondari ya Nyakusungwa zilivyotolewa na Airtel wakati wa uzinduzi wa manara huo kwaajili ya kuwawezesha wakazi na wanafunzi kutoka katika maeneo hayo kupata nyenzo muhimu katika kuboresha elimu na kutatua changamoto za vitabu zinazoikumba shule hiyo ya sekondari Kuzinduliwa kwa minara hiyo ya Nyakasunga wilaya ya Sengerma Mkoani Mwanza na kijiji cha Chikobe mkoani Geita ni mpango mkakati wa Kampuni ya Airtel Tanzania kufikisha mawasiliano kote nchini hasa katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa nchi