Mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akiwa amembeba mjukuu weke. Kulia ni Zari
MPENZI wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Zarinah Hassan ‘Zari’ amejifungua mtoto wa kike leo alfajiri saa 10: 40 jijini Dar es Salaam. Mtandao huu umeongea na Meneja wa kimataifa wa Diamond Platinumz, Salam Sharaf ambaye amethibitisha taarifa hizo na kusema Zari bado yupo hospitali mpaka sasa.
Kutokana na usumbufu aliodai unaweza kutokea, Salam hakuweka wazi hospitali aliyojifungulia Zari. “Ni kweli Zari kajifungua mtoto wa kike majira ya saa 10 alfajiri leo, lakini kutokana na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sasa siwatajii hospitali aliyojifungulia mpaka hapo baadaye” Alisema Salam.
Kupitia akaunti za mitandao ya kijamii, Diamond Platnumz amemkaribisha duniani binti yake huyo aliyemuita Tiffah kwa kuandika hivi: Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya moyo wangu… karibu kwenye ulimwengu
Maneno hayo yaliambatana na picha ya mama yake mzazi aitwaye, Sanura Kassim ‘Sandra’ anayeonekana akiwa amembeba mjukuu wake hospitali. Pembeni ya picha hiyo yupo Zari.
Mtandao huu unatoa pongezi wa Diamond pamoja na Zari kwa kupata mtoto wa kike