MSIBA! Staa mwenye umri mdogo anayekimbiza katika filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata pigo baada ya kufiwa na bibi yake mzaa mama, Leonadina Mboneko, aliyefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Masana, iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Amani mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila alisema mama yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu jambo lililomlazimu kumtoa nyumbani kwake Bukoba na kumleta jijini kwa ajili ya kupata matibabu.
“Nimehangaika naye kwa muda mrefu ili kurejesha afya yake, lakini hali ilikuwa ngumu hadi juzi Mwenyezi Mungu alipomchukua. Tumepata pigo kubwa sana hasa mwanangu Lulu kwa sababu alikuwa ndiye kipenzi chake,” alisema mama huyo.
Muigizaji huyo aliyecheza Filamu ya Foolish Age hakuweza kupatikana kuzungumzia msiba wa kipenzi chake huyo, lakini nyumbani kwa mama yake, mipango ya kusafirisha mwili huo kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya mazishi ilikuwa ikifanyika