WASANII zaidi ya 100 wa muziki na filamu leo Agosti 6, 2015 wanakusanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa chakula cha jioni sambamba na ‘live performance’ kwa ajili ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika hafla hiyo, wasanii watapata fursa ya kumuaga Rais Kikwete anayemaliza kipindi chake mwaka huu, kumshukuru kwa kushirikiana nao katika miaka yake 10 kama Rais kwa kukuza tasnia yao na pia kumkaribisha Mgombea urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli.