Chumba maalum cha mtoto wa Diamond Platnumz.
Staa wa Bongo Fleva
Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mama kijacho wake, Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wameandaa chumba maalum cha mtoto wao wa
kike ajaye na kuweka vifaa na vitu vya gharama kubwa.
TUJIUNGE ‘WHITE HOUSE’
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na familia
ya Diamond, baada ya kutenga chumba hicho maalum kwenye ‘White House’ ya
rais huyo wa Wasafi Classic Baby (WCB) iliyopo Madale-Tegeta jijini
Dar, kilichofuata ni kukinakshi kwa vitu hivyo vya gharama
vilivyonunuliwa Afrika Kusini ‘Sauzi’, Dubai na London, Uingereza.
ETI KIMEPAKWA MADINI
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba, pamoja
na vitu vingine lakini chumba hicho kina kitanda spesho cha mtoto huyo
ambacho kimepakwa madini (hakutaja ni madini ya aina gani).
“Wewe fikiria, kama toileti kwake ameweka vitu vya madini inashindikana nini kwa mtoto wake mtarajiwa?
ANATAKA AMFUNIKE KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST
“Unajua watu hawajui lakini Diamond ana
shauku ya mtoto hadi anapitiliza so anataka mwanaye hata amfunike yule
North (mtoto wa kike wa mastaa wakubwa wa Marekani, Kim Kardashian na
Kanye West) ndiyo maana amejaza makorokoro kibao.
DAZENI KWA DAZENI
“Mbali na hivyo, kuna vitaulo, nepi,
pempasi, vitambaa na vichupi vya mtoto dazeni kwa dazeni, mafuta na poda
za mtoto, tishu na pini ambavyo vimejazwa kwenye vikabati maalum
ambavyo haviingizi mavumbi.
“Pia chumba hicho kina midoli mizuri ya
mtoto iliyopamba masofa yaliyopo ndani ya chumba hicho ambacho
hakiruhusiwi mtu mwingine kuingia zaidi ya Zari na Diamond,” kilisema
chanzo chetu hicho.
GHARAMA MIL. 10
Sosi wetu huyo alifunguka kuwa, ukiacha
kitanda, masofa, gharama ya utengenezaji, vikokoro vyote vinagharimu
zaidi ya Sh. milioni 10 za Kitanzania.
“Unajua vitu ni vingi na jamaa (Diamond)
huwa ananunua kila kukicha ‘so’ sidhani kama anaweza akawa na ‘figa’
kamili ila kwa nguo na vitu vingine vidodovidogo si chini ya milioni
kumi,” alisema sosi huyo kwa sharti la kutochorwa gazetini kwa kigezo
kuwa si msemaji wa familia.
HUYU HAPA DANGOTE MWENYEWE
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti
hili lilimsaka Diamond au Dangote au Chibu kama Zari anavyopenda kumuita
kisha kumuuliza juu ya gharama za chumba hicho ambapo alifunguka:
“Wewe ujue tu kuwa ni chumba cha gharama kubwa.
KAMA SHILINGI NGAPI?
“Vitu vingi sijanunua hapa (Bongo) na sijafanya calculations (mahesabu).
WATU WANASEMA NI KUFURU, WEWE UNASEMAJE?
“Dah! Ukweli gharama ni kubwa sana
iliyotumika kukiandaa chumba cha baby girl wangu, mimi siyo wa kwanza
Tanzania na duniani kununua vitu kama hivyo japokuwa kuna watu watabeza
na kuongea wanachotaka.
SASA MBONA MTOTO BADO NA SIKU ZIMETIMIA?
“Hiyo ni mipango ya Mungu, mashabiki wangu wamuombee Zari ajifungue salama muda wowote.”