Baba wa Kim Kardashian ambaye kwa sasa amebadili jinsi yake na kuwa mwanamke, ‘Caitlyn Jenner’.
New York, MarekaniBABA wa Kim Kardashian ‘Caitlyn Jenner’ ambaye kwa sasa amebadili jinsi yake na kuwa mwanamke anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa sauti ili awe mwanamke aliyekamilika.
Akizungumza na mtandao unaodili na habari za mastaa, Caitlyn alisema kuwa alifanyiwa upasuaji wa kila kitu na kuwa mwanamke kwa muonekano lakini sauti yake bado ilikuwa haijabadilishwa ili kumpa sifa ya kuitwa mwanamke.
“Kila kitu nimefanikiwa isipokuwa sauti tu na hivi karibuni nitafanya operesheni, nashukuru watoto wangu lakini zaidi ni Kim Kardashian ambaye ananisapoti kwenye kila kitu,” alisema