Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa na mkewe Josephine Mushumbushi.
Mwandishi Wetu
IMEVUJA! Siri ya kitu
kilicho kichwani mwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Dk. Wilbroad Slaa kuhusu mustakabali wake wa kisiasa umedaiwa
upo kwa mkewe, Josephine Mushumbushi, Ijumaa Wikienda imevujishiwa.
Dk. Wilbroad Slaa.
Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na
mwanasiasa huyo, kimeliambia gazeti hili kuwa mke wa kiongozi huyo
mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania, anafahamu uamuzi
uliochukuliwa na mumewe, isipokuwa kinachosubiriwa ni siku ya kutoboa
kwa Watanzania.
“Dk. Slaa ameshachukua uamuzi wake na
mtu pekee anayefahamu alichokifikia ni mkewe, kinachosubiriwa hapa ni
siku tu ya kuwahabarisha Watanzania, lakini kama kuna mtu zaidi mwenye
kujua kwa kina mwisho wa suala hili kwa sasa ni mkewe,” alisema mtoa
habari huyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Alipotafutwa Dk. Slaa ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu yake haikupatikana. Jitihada zinaendelea.
Sakata la Dk. Slaa na chama chake lilijitokeza baada ya Chadema kumkaribisha waziri mkuu aliyejihuzulu, Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho na kuteuliwa kuwania urais kupitia muungano wa Ukawa.
Sakata la Dk. Slaa na chama chake lilijitokeza baada ya Chadema kumkaribisha waziri mkuu aliyejihuzulu, Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho na kuteuliwa kuwania urais kupitia muungano wa Ukawa.
chanzo: GPL