Meneja wa
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akifafanua jambo kwa
kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), kabla ya kumkabidhi msaada wa
Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa
Arusha jana. Wanaoshuhudia ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence
Tarimo (kushoto) na maafisa wa Airtel wa Mikoa ya Arusha na Manyara.
Meneja wa
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikata utepe kuashiria
kumkabidhi kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), msaada wa Zizi jipya
na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa
Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana
huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli,
Polas Emmanuel.
Meneja wa
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimpongeza Jonathan
Tarimo (wa pili kulia), baada ya kumkabidhi msaada wa Zizi jipya na
Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’,
katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana.
Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence
Tarimo, Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel na
Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara, Peter Kimaro.
Meneja wa
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa tatu kushoto), akikabidhi
Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada
wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango
wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’
wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni
Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa
Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel.
Meneja wa
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa
maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe
wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel
‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli
mkoa wa Arusha jana.
AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”
imemkabidhi kijana Jonathan Clement mkazi Migungani kata ya Mto wa
Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha ng’ombe wawili, banda la kisasa
pamoja na mafunzo ya biashara ambayo itamsaidia kuinua biashara yake
ya ufugaji na kumuongezea kipato chake.
Jonathan kijana
mwenye umri wa miaka 21 na elimu ya kidato cha nne amekabidhiwa mtaji
huo ambapo awali alikuwa na ngomb’e wawili na banda lililochoka na
alikuwa na changamoto ya elimu ya ufugaji na madawa ya mifugo.
Jonathan
ameishukuru kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kumpatia msaada
huo amesema “biashara yangu ya ufugaji sasa itapiga hatua. Naamini
miaka michache ijayo nitakuwa na mifugo mingi sana na soko langu la
maziwa litakuwa kwa kasi. Na vile vile itaniwezesha kuinua familia na
biashara yangu kwa ujumla”.
“Hii ni bahati ya
peke kwangu kutoka Airtel, kwani ni vijana wengi sana wanatamani kupata
hivi nilivyovipata lakini hawakupata bahati hii. Nawahimiza vijana
wengine wasikate tamaa na wajitokeze kwa wingi kwani Airtel Fursa ipo
kutuwezesha vijana”.
Akizungumza baada
ya makabidhiano, Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa
Bayumi, alisema “mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na
kuwakwamua kiuchumi. Jonathan amepitia changamoto nyingi kufikia hapa
alipo alianza na ngombe wa kukopeshwa kutoka kwa mjomba wake kwa
makubaliano kwamba atakapopata ndama wa kwanza atakuwa wa kwake. Lakini
leo hii tumemuwezesha kuwa na jumla ya ng’ombe watatu kwenye zizi lake”.
“Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha”
imempatia msaada huu Jonathan baada yakuridhishwa na hatua ya ufugaji
pamoja na kuonyesha nia yakuwa mfugaji bora hapa nchini” alisema.
Bayumi aliwataka
vijana wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huu unawalenga
vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa
au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao..
“Program hii inahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini alisema.
Ili kijana
kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi
kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com<mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>
ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.
Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya
Airtel www.airteltanzania.com