Aug 13, 2015
Mashabiki wavutana kuhusu Alikiba kuwekwa kipengele cha ‘Msanii Mpya wa Mwaka’ tuzo za AEA USA 2015
Muimbaji huyo wa ‘Chekecha Cheketua’ anawania kipengele kimoja na wasanii kama Mc Galaxy (Nigeria), Jodi (Nigeria), Phyno (Nigeria) na wengine.
Alikiba ameandika Instagram “Vote Vote Vote For Alikiba Link Iko Hapo Juu” kuwahamasisha mashabiki wake waendelee kumpigia kura.
Ili kumpigia kura Alikiba kipengele cha Msanii Mpya wa Mwaka tuzo za AEA USA ingia hapa.
Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki wa muziki waliovutana, wengine wakihoji kwanini amewekwa katika kipengele asichostahili na wengine wakijaribu kuwa na mitazamo tofauti.