Vanessa Mdee aliwekwa kwenye Kikaango cha EATV wiki hii ambapo
mashabiki wake walipata fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali yakiwemo
ya uhusiano wake na Jux na mipango yao ya baadaye.
Akijibu swali la mipango aliyonayo na Jux, muimbaji huyo alisema
wanatarajia furaha ya kudumu huku akidai kuwa hawana mpango wa kuwa na
mtoto siku za hivi karibuni.
Pia Vanessa alidai kuwa amekuwa na uhusiano na Jux kwa mwaka mmoja na miezi minne sasa.
Kuhusu collabo ba Diamond, Vee Money alisema itakuwepo muda si mrefu na anaamini kuwa itakuwa ya kuotea mbali.
Kuna mtu alimuuliza kama ana beef yoyote na Alikiba na Vanessa
kujibu, “Ali Kiba sina beef naye infact sina beef na mtu yeyote.
Nampenda nakumheshimu sana. Hatujawahi kufanya kazi ya mziki pamoja
lakini ninamuamini sana ana kipaji sanaa na cha kipekee. Tunashirikiana
kupinga ujangili kama mabalozi wa Wild Aid.”
Kuhusu kama bado anaendelea kufanya kazi na MTV Base, Vanessa
alijibu, “Mdee Nimeacha kufanya vipindi vya kawaida nafanya vipindi
maalum tu kama interview ya Neyo nilioifanya katika tuzo za MAMA 2015.”
source: Bongo5