MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Aug 13, 2015

Rockstar4000 watangaza ujio wa collabo ya Alikiba na Ne-Yo


page
Kampuni inayomsimamia Alikiba, Rockstar4000 imetangaza kuwa msanii huyo atamshirikisha msanii wa Marekani, Ne-Yo. Imetoa tangazo hilo kupitia Instagram.
“Exciting News: African superstar Alikiba will be collaborating with International Superstar Ne-Yo — More news to follow…. #kingkiba #ROCKSTAR4000,” imeandika.
Ne-Yo ambaye alitumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu, anatarajia kuja tena Afrika hivi karibuni ambapo ataungana na wasanii waliopo kwenye kipindi cha Coke Studio Afrika jijini Nairobi, Kenya.
Alikiba ni miongoni mwa wasanii waliopo kwenye msimu huo mpya.
Album mpya ya Ne-Yo Non-Fiction ilifika namba moja kwenye chati ya Billboard’s Top R&B/Hip-Hop Albums.
Pamoja na Ne-Yo, Alikiba pia anatarajia kumshirikisha msanii wa Nigeria, Davido.