MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Aug 3, 2015

Nisha awekwa chini ya ulinzi China

nishaa 
Staa wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’.
Hamida hassan
Yamemkuta! Staa wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’ ameonja joto ya jiwe baada ya kuwekwa chini ya ulinzi mkali huko Hong Kong, China ambapo alidhaniwa kuwa amebeba madawa ya kulevya ‘unga’.

nishaAkizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Nisha alisema kuwa alijikuta akiichukia nchi ya China baada ya kupata wakati mgumu alipowekwa chini ya ulinzi kwa muda wa saa nne.
“Yaani China si mchezo, ukienda uwe na sababu, bila sababu unaweza kujikuta unaishia jela, kwa sasa Watanzania hatuaminiki kabisa, mwenzenu nilikamatwa na kupekuliwa mpaka walipojiridhisha ndipo wakaniachia,” alisema Nisha