Sstaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Imelda Mtema
Stop! Wakati akisubiriwa kujifungua muda wowote, mwandani wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anadaiwa kuwazuia baadhi ya ndugu wa jamaa huyo kuingia kwenye chumba maalum kilichoandaliwa ili kuepuka kisiingie vumbi na kiwe safi wakati wote.

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Chanzo chetu ambacho ni mmoja wa ‘memba’
wa familia hiyo kilipenyeza kuwa, kwa sasa nyumbani kwa mwanamuziki
huyo maeneo ya Madale-Tegeta, Dar, wana bashasha wakimsubiria mtoto huku
chumba hicho kikiwekewa uangalizi mkubwa.
“Yaani Zari hataki mchezo kabisa na
haruhusu mtu kuingia chumbani humo hovyo kwa sababu ya kuepuka vumbi kwa
mtoto kwa maana chumba hicho hakihitaji msongamano wa watu wengi,”
kilisema chanzo hicho.
Mpashaji huyo aliweka wazi kuwa, Zari
alitia ngumu na kusema ni sheria aliyoiweka mwanamama huyo na haitakiwi
kukiukwa na mtu yeyote kwa kuwa wanafahamu fika kuwa chumba cha mtoto
hakihitaji msongamano wa watu hivyo ndugu hao imebidi wawe wapole.
Kilidai kwamba, kwa sasa kila mtu
anayefika nyumbani hapo anahojiwa na kwamba kama siyo ndugu wa ndani
zaidi kwenye familia haruhusiwi hata kuingia getini.Akizungumza na
Ijumaa Wikienda kuhusu maandalizi hayo, Diamond alisema kila kitu kipo
sawa na kwamba, anamuomba Mungu mambo yaende kama alivyopanga.
chanzo gpl