Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya Ushindi wa Tatu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ambaye alipokea kwa niaba ya
Ofisi ya Uhamiaji walioibuka washindi wa tatu katika Maonesho hayo ya
Kilimo Nane nane yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi.
Wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji
wakiwa katika Picha ya Pamoja wakishangilia Ushindi walioshinda katika
Maonesho ya Kilimo ya Nane nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi na
Kufungwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Afisa Uhamiaji Mkoa waLindi
Abdallah Towo akiwa na Martin Mhagama,Mkaguzi wa Uhamiaji Lindi wakiwa
wameshikilia kikombe cha Ushindi wa Tatu walichokabidhiwa na Rais
Kikwete katika Maonesho ya Nane nane
Mratibu wa Uhamiaji kutoka Makao
makuu Bi. Tatu Burhani (mwenye Hijabu) akiwa sambamba na Sofia Maunda
ambaye ni Konstebo wa Uhamiaji Lindi (mwenye Kofia) wakiwa katika Banda
lao la Maonyesho katika sherehe za Nane nane Mkoani Lindi.