Aug 11, 2015
Umoja wa mataifa wadai hadi mwaka 2100 dunia itakuwa na watu bilioni 11, nusu watakuwa Afrika
Utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa umebaini kuwa hadi kufikia mwaka 2100, idadi ya watu duniani itafika bilioni 11 ambapo nusu yake watakuwa barani Afrika..Umesema kuwa hadi mwaka 2050 idadi ya watu duniani itaongezeka kutoka watu bilioni 7.3 hadi watu bilioni 9.7 na hadi mwaka 2100, idadi ya watu bilioni 1.2 waliopo Afrika itaongezeka hadi kufikia bilioni 5.6.
Wataalam wamesema ongezeko hilo la watu litasababisha kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira, kukosekana na rasilimali na mafuta, ukosefu wa ajira, umaskini, uhalifu na machafuko ya kisiasa.
Utafiti huo uliwasilishwa na John Wilmoth, mkurugenzi wa kitengo cha idadi ya watu cha Umoja wa Mataifa kwenye mkutano uliofanyika nchini Marekani.
Chanzo: Daily Mail