Aug 11, 2015
Bado siamini kama TID anatumia unga – Jay Moe
Rapper Juma Mchopanga maarufu kama Jay Moe amesema bado inamuwia vigumu kuamini kuwa rafiki yake TID anatumia madawa ya kulevya..Jay Moe amekiambia kipindi cha jana cha Mkasi kupitia EATV kuwa ingawa anasikia tetesi kuwa TID anatumia unga, bado hajawahi kumuona hata siku moja.
“Hata inaniwia vigumu kuamini TID anatumia hiki kitu kwa sababu kila siku tunaenda studio, sioni moment fulani kanikimbia yaani kaenda kajiiba karudi, ana behave tofauti dakika kumi na tano za nyuma,” alisema Jay Moe.
“Hivi karibuni tulikuwa tunaandaa project yetu ya wasanii wa Kusini tunarekodi naye na hakuna kitu kama hicho na msikitini tunaenda kwahiyo nabaki tu nisije nikapata dhambi kwamba huyu jamaa anafanya hiki kitu kumbe hafanyi,” alisisitiza.
“Mimi naona hao ambao wanahisiwa wanatumia kama kweli wanatumia, isije ikafikia hatua mbaya ndio wakaja kujitokeza kwenye jamii na kusema kwamba ‘kweli mimi nilikuwa nafanya’, wengi wao mimi naamini hata ukiwaweka kwenye hiki kiti nilichokaa na ukiwauliza wewe ‘bwana kweli unatumia’ atakwambia hapana! Vijana wengine wanahisi wakitumia wataendelea na ustaa wao na maisha yakawa vizuri.”