MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Aug 11, 2015

Video Mpya Ya Jux ‘Looking For You’ Ft. Joh Makini Iliyoshutiwa S.A Kutambulishwa Exclusive Na MTV Base (August 11)


Jux Mtv Base
Jux anatambulisha video mpya ya wimbo aliomshirikisha rapper Joh Makini, ‘Looking for you’ leo August 11..Video hiyo iliyoshutiwa Afrika Kusini na kuongozwa na Justin Campos wa Gorilla Films itaoneshwa kwa mara ya kwanza (Exclusive) na MTV Base saa 12 kamili jioni saa za Afrika Mashariki.
“Kwa wapenzi wa mziki mzuri, muda ni saa kumi na mbili jioni, channel ni @mtvbaseafrica ( DSTV 322) siku ni jumanne tarehe 11 August 2015. I’m #LookingForYou @Juma_Jux ft @Joh_Makini produced by @Nahreel #TheIndustry and the rest is history.” ameandika Jux kwenye Instagram yake.
Mapema mwaka huu Jux, Vanessa Mdee, Joh Makini, G-Nako Nahreel na Aika walienda Afrika Kusini kufanya video na Justin Campos, ‘Looking For You’ ni miongoni mwa video zilizofanywa wakati wa safari hiyo. Zingine ni ‘Nusu Nusu’ ya Joh Makini na ‘No Body But Me’ ya Vanessa.

credit: Bongo5