Msimu wa pili wa Kwetu House - “kwetu house, kipaji zaidi ya soka” shindano ambalo hujumuisha zaidi wapenzi wa soka wenye Kipaji, jumla ya mikoa sita (Arusha, Zanzibar, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam) kutoa
washiriki zaidi kwa ajili ya kunogesha na kuleta upinzani wa kutosha
msimu huu mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 15, tofauti
na msimu uliopita ambao ilikuwa Sh milioni 10.
Safari
ya Kusaka Vipaji kwa Mashabiki wa Kweli wa Soka inatia nanga Dar es
Salaam Msimu huu wa Pili ni siku Mbili za Kuonyesha Kipaji kwa Wakazi wa
Jiji Kubwa la Dar es Salaam. Tarehe 6 na 7 Mwezi wa 8 Kwenye Uwanja wa
Taifa Temeke.Uwe ni Mwigizaji,Mchekeshaji, Mchoraji,Mtangazaji wa Radio/Tv,Mbunifu wa Mavazi,Mwimbaji kazi ni kwako KWETU HOUSE 2015 Msimu wa Pili ni VIPAJI NA SOKA.
Washiriki
wa Kwetu House 2015 Msimu wa pili kutoka Arusha, Zanzibar na
Dodoma,Mbeya, Mwanza wataungana na Washiriki kutoka Dar es Salaam
kushindania Milioni 15.