Meneja
Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati),
akiwakabidhi wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO mjini Mbeya vifaa
mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa nyuki.
Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa
mizinga ya nyuki, mashine za kukamulia asali, vifaa vya kinga ya nyuki
na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki. Wakishuhudia
kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na
Meneja mauzo wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani
Meneja
Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiongea
na wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO katika hafla fupi ya makabidhiano
ya vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa
nyuki vikiwemo mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa
vya kinga ya nyuki 2, chupa za lita 1 400, chupa za asali za lita 5,
200 na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki mjini
Mbeya . Wakishuhudia kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA
Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani.
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Airtel imewawezesha vijana wajasiriamali wa
kikundi cha MINARACO kutoka mkoani Mbeya wanaojishughulisha na ufugaji
wa nyuki. Kikundi hicho kinaundwa na vijana 76 walioamua kuungana na
kujihusisha katika ufugaji wa nyuki ili kujikwamua na changamoto za
maisha. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa
kupatiwa mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya
kinga ya nyuki 2, chupa za lita 1, 400, chupa za asali za lita 5, 200 na
zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki
Akikabidhi
vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi
alisema, “vitendea kazi waliopatiwa ni vyakisasa zaidi na vitasaidia
kuboresha ufugaji huo na kuwawezesha vijana hao kupata mavuno zaidi ya
waliokuwa wakipata awali”.
Akiongezea
amesema, “mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni sehemu ya
mpango wa kampuni ya Airtel wa kuwawezesha vijana ili kuboresha maisha
yao na ya watu wanaowazunguka”.
“Sisi
kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na
wajasiriamali na hasa vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ili
kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo
na vifaa” alisema meneja huyo”.
Wakipokea
msaada huo wameishukuru, Airtel kwa kujitoa kwa kuwasaidia vijana
katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuahidi kutumia vifaa hivyo
kwaajili ya kuongeza uzalishaji ili kufikia malengo waliojiwekea katika
kikundi hicho.
“Hatukuamini
kuwa Airtel itakuja kututembelea, kuangalia mahitaji yetu na hasa kwa
kutupatia msaada wa vifaa vya kisasa walivyo tupatia leo, tunawashukuru
sana na tunaahidi kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha tunakuza na
kuendeleza ufugaji bora wa nyuki” alisema mwakilishi wa kikundi hicho
John Maige.
Akiongezea
Maige alisema, “Awali tulikuwa na changamoto ya uchache wa mizinga,
vifungashio vya asali na soko la uhakika, lakini Airtel imetusaidia kwa
kutupa mafunzo na vifaa vya kutosha vitakavyo tusaidia kupata Asali ya
kutosha na yenye ubora mzuri “.
Kampuni
ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la
kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana.